Aunt Rahma Shopping Centre

Aunt Rahma Shopping Centre
Kariakoo/Tabata Muuzaji wa nguo mbalimbali za watoto na wakubwa kwa bei poa kutoka China na Dubai

Jumatatu, 12 Oktoba 2015

Historia ya Mwanariadha maarufu asiyeona-Kenya

Makala

Historia ya Mwanariadha maarufu asiyeona



Henry Wanyoike  aliyezaliwa  mwaka 1974  ni Mwanariadha wa Kenya asiyeona. Anashiriki katika mashindano ya Paralympics  shindano la Marathon.

Wanyoike ni mmoja wa Wanariadha wa kasi sana duniani. Alianza kukimbia akiwa mtoto na tayari alikuwa na ndoto ya kujiunga na kundi la Kenya la wanariadha.

 Nchi hiyo  inajulikana kwa kuwakuza Wanariadha wengi wa Masafa marefu wa Kimataifa kuliko nchi nyingine yoyote.

Alitia fora katika mita 5000 na mita 10,000.

Mnamo 1995, Wanyoike alikuwa kipofu wakati alipata mshtuko. Alisimulia,alieleza kwamba alienda kitandani akiwa mzima, kuamka aliona giza machoni pake. Usiku huo alipoteza karibu asilimia 95 ya uwezo wake wa kuona na polepole akiupoteza wote. Alifikiria akaona maisha yake yamefika kikomo.

Mamaye Grace alimchukua katika kliniki ya macho ya Kikuyu inayotambulika kama moja ya vituo bora zaidi vya watu walio na shida ya macho katika eneo la Afrika Mashariki.

Msimamizi wa mradi wa Low Vision alimsaidia kujipanga tena kimaisha na akampanga kujifunza kushona fulana. Kwa shukrani kubwa alikubali mradi huo na kuahidi kuwasaidia vipofu wengine kujitegemea kimaisha .

Baada ya kushinda Nishani ya Dhahabu kule Sydney, Australia katika Mashindano ya Paralympic ya 2000, Wanyoike amenunua mashine nyingi za kushona kutokana na zawadi ya fedha alizokabidhiwa na watu maarufu kama vile Arnold Schwarzenegger. Akawa  ni mwajiri wa watu wengine vipofu wa Kenya na kuwafundisha kufuma fulana.

Mwanariadha kopofu huwa na mtu wa kumwongoza aliyefunganishwa naye mkononi. Kiongozi hutumia kiunganishi hiki kumwashiria mwanariadha, bila kumzidi kasi, wakati wa kugeuka, kupunguza kasi na kuhepa kizuizi, iwe kiwanjani au barabarani.

Henry alipozoea kushirikiana na viongoza, alichipuka haraka kama mwanariadha kipofu wa kimataifa.

Vichekesho vya Mtandao


Vichekesho vya Mtandao


Mmasai na mwanajeshi walikuwa
wanapigana yule masai akamrushia
mwanajeshi mkuki .Mwanajeshi
kutokana na mazoezi ya kijeshi
akaudaka ule mkuki na kuuchoma
chini pembeni ya miguu yake, kisha
akatoa bomu na kumrushia masai
yule mmasai nae akalidaka bom nae
kuonesha mbwembwe akalitupa
chini ya miguu!!!
kilichofata cjui manake me
nilikimbia......

Nimeipenda hiyo!

Peruzi-Magazeti


Peruzi -Magazeti





Jumapili, 11 Oktoba 2015

Safari ya Bagamoyo


Safari yangu ya Utalii wa ndani

Kaole- Bagamoyo, Pwani




 

 

Bagamoyo ni Wilaya iliyopo ndani ya  mkoa wa Pwani, Nchini Tanzania, Afrika Mashariki.

 

Wilaya hii inasifika kwa historia ya Mambo ya Kale ikiwemo vivutio vya kitalii. Wakoloni walikuwa wakifanya biashara ya  watumwa.

 

 

Jina la Bagamoyo katika historia yake halisi ilikuwa ni Bwagamoyo . Lakini Baada ya Mzungu kushindwa kutamka, Aliita Bagamoyo. Jina likakua hadi leo.

 

Ni eneo lililopendwa  na wafanyabiasha wa utumwa hapo kale, kama kituo chao cha mapumziko na kubwaga moyo.

 

 Moja ya kivutio nilichokuwa nakitamani kuona baada ya kupata historia yake  ni eneo la  Kaole lenye historia ya kusisimua.

 

Nikiwa mwana habari na mwandishi wa Vitabu, sikupenda hata kidogo kupita bila kuhabarisha na kubaki kumbukumbu katika kitabu. Nilihitaji nishuhudie kwa macho yangu eneo hilo na kulifanyia kazi ndani ya nakala zangu.

 

Kwa bahati nzuri nilipata likizo fupi ya Sikukuu, hapo ndipo nami nilipotumia nafasi hiyo nikiwa na familia yangu kudhuru eneo la Kaole.

 

Haikuwa mwendo mrefu kutoka Dar es salaam mpaka Bagamoyo. Hatimaye nilifika kaole na kujionea maajabu ya vitu vya kale na historia yake.

 

Ufikapo  unakaribishwa kwa bakshasha na waongozaji wa eneo hilo la kihistoria. utapelekwa sehemu maalumu ya wageni,yenye viti vilivyopo chini ya mti.

 Utaelezwa historia ya Kaole ikifuatiwa na kuelekea sehemu moja baada ya nyingine kwa ajili ya kujionea maajabu ya mambo ya kale.

 Kuna vitu vingi vya kushangaza ikiwemo majengo ya kale, msikiti uliojengwa kwa mawe, Vyombo mbalimbali vilivyokuwa vikitumika zamani.

 

Nilivutiwa zaidi na historia ya Kaburi la wapendanao. Kaburi hili lilikuwa la mke na mume ambao walikuwa Wanapendana sana. Pia wakishirikiana katika biashara.

 Wakati walipokuwa katika harakati za safari ya kibiashara chombo chao kilizama.  Historia yao inasema kutokana na mapenzi ya dhati waliyonayo, waliamua kujifunga nguo pamoja ili kama kufa wafe pamoja. Wakafariki wote wakiwa wamejifunga nguo hiyo.

 Watu waliopoa miili yao ikiwa imejifunga pamoja. Kwa heshima waliamua kuwazika pamoja kama ambavyo waliona walivyojifunga. Japo Kaburi lilikuwa moja lakini kila mmoja alizikwa mwanadani wake.

Kufuatia historia ile tangu wakati ule mpaka leo, mume na mke au wachumba, wamekuwa wakienda pale kujiapiza katika ndoa au mapenzi yao yasivurugike. Awe Mwafrika, Mzungu n,k wamekuwa na imani ya kupata mapenzi ya dhati wajiapizapo katika kaburi la wapendanao

 

Maji ya ajabu

 Kuna kisima ambacho kimekuwa ni kivutio. tangu  karne na karne lakini hakijawahi kukauka. Hakina maji mengi, Ila unaweza ukachota ujaze mapipa  uwezavyo, bado maji yale yasihisi kupungua. Si mengi ukiyaona wala kisima si kirefu, lakini hayaishi.

Ajabu ya maji yale yapo karibu na bahari ila yenyewe ni baridi hayana chumvi hata kidogo. Unaweza kunywa na kufanyia utakacho.

 Maji hayo yamekuwa yakiheshimiwa na kutukuzwa sana.Wakiamini ni maji ya baraka.  Wengi huenda kwa ajili ya kuyachota ili kuyaoga waondoe matatizo yao.

 Kaburi la Msichana mtabiri

 Katika historia yake kulikuwa na msichana mdogo, alikuwa mtabiri wa mambo mbalimbali. Watu walikuwa wakitabiriwa mambo yajayo ambayo walikuwa wakiyaona baada ya utabiri huo.

Utabiri wake ukampa umaarufu katika umri mdogo. Akiwa na Umri wa miaka 14 alifariki ghafla, ikafuatiwa na watoto wengine kufariki ghafla katika siku aliyofariki binti huyo. Kutokana na imani waliyonayo, walimzika yule binti na pembeni yake waliwazika  Wale watoto watatu wakiamini ni malaika.

Sehemu hiyo, pia watu wamekuwa wakienda kuomba ili kuondokewa na matatizo mbalimbali.

 

 Mbuyu wa ajabu

 Mbuyu huu unaambiwa kuna upande mmoja ukizunguka unaongeza siku za kuishi na upande mwingine ukizunguka, unapunguza siku za kuishi. Wengi wamekuwa wakienda pale tangu enzi za kale ili kuzunguka.

Kitu kingine katika  mbuyu huu umekuwa ukigongwa misumari mingi na watu toka enzi za zamani mpaka leo. Huamini wanapoigongelea misumari katika mbuyu ule husamehewa dhambi zao. Mbuyu huo una miaka mingi sana na misumari mingine imekuwa tayari imeanza kufunikwa na magome.

Bandari  ya kale

Upande wa chini katika eneo hilo la Kaole kulikuwa na kivutio cha bandari kuu  hapo kale. Lakini haikuendelezwa ili kuikuza historia hiyo. Mikoko bado inaonekana kuwepo. Kwa sasa maji yakipwa na kujaa huingia eneo hilo japo si mengi kama awali.

 Bagamoyo kuna mambo mengi ya kuvutia. Njia zake za zamani,huwa ni kivutio. Maeneo mengi hufanana na yale ya visiwani Zanzibar.

 

                                         Livingstone hotel

 


 

                                                Kaole

 


                                         

Bagamoyo-Pwani
Tanzania
East-Africa
 

Jumatatu, 13 Julai 2015

Kwaheri- Benson Wanjau "MZEE Ojwang"
Gwiji la vichekesho -KENYA
 Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, alifariki jana.Alikuwa amelazwa Kenyatta national hospital,akisumbuliwa na ugonjwa wa pneumonia.
 Tutamkumbuka daima kwa umahiri wake katika sanaa ya vichekesho.
Kipindi cha Vitimbi kimepata pigo.

Pole sana Mama Kayayi.



Jumapili, 12 Julai 2015

Ni Magufuli Ccm. "JEMBE."Mchapakazi....













Anafahamika kama "JEMBE " ukipenda wanamwita "Tingatinga"

Utendaji na umahiri wake katika kazi na kujiamini. Turufu ya Ccm ktk safari ya Oktoba.

Hongereni kina mama mlio ingia ktk kinyang'anyiro hicho hadi  3 bora. Dr Asharose Migiro aliyonitoa nikafahamika ndani na nje ya nchi kama mwandishi wa Vitabu Mwanamke,baada ya kunizindulia Vitabu vyangu 14,akiwa Waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia na watoto.
 TAMWA wakiratibu uzinduzio huo, idara ya habari Maelezo.

 Hongera mama Samiya Suluhu Hassan. Ukiwa Ni Mwanamke wa kwanza, kushika nafasi ya Makamu wa rais Tanzania kupitia Ccm.Kila la heri nyote katika kutimiza malengo yenu. Pale Oktoba.

Namkumbuka Mh. Samiya, akiwa Waziri wa Wanawake na Watoto Znz, niliwahi kumualika katika Semina ambayo nilikuwa naratibu
juu Uwandishi wa Vitabu vya fasihi katika kuelimisha gonjwa la UKIMWI. Ilikuwa mahususi kwa Wanawake Waandishi Zanzibar.Asilimia kubwa ya washiriki walikuwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Zanzibar.

Alihudhuria na kutoa mchango mkubwa wa mawazo katika shughuli hiyo.

Hongera Balozi Amina kwa nafasi nzuri hatimaye kushika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro cha urais.Hakika umeonyesha mfano mzuri kwa Wanawake wa Visiwani na bara ktk kujiamini.

 Kila la heri mnapoendelea na safari yenu kuelekea Oktoba.

Wanawake wanaweza.






Jumanne, 16 Juni 2015

Siku ya Mtoto wa Afrika 2015

 
 

Siku ya Mtoto wa Afrika

 

 

“Kuondoa Mila zenye kuleta madhara ni jukumu letu sote”.

 

Tarehe 16 juni mwaka 1976 Nchini Afrika ya kusini katika kitongozi cha soweto,kulitokea mauaji ya kikatili dhidi ya watoto nchini humo,watoto hao waliouwa wakiwa katika maandamano yaliyokuwa na lengo la kupinga agizo la serikali ya makaburu wakati huo,lillilotaka wanafunzi wafundishwe masomo katika lugha ya kiafrikana badala ya kingereza.

 Watoto  walipinga kufundishwa katika lugha ya kiafrika kwa sababu lugha kiafrikana haizungumzwi na kueleweka mahali popote duniani,zaidi ya Afrika ya kusini tu.

Watoto hao waliona pia lugha hiyo ingeweza kuwakosesha ajira katika nchi nyingine duniani.

 maandamano yao yalitawanywa na polisi wa makaburu kwa kuwatupia mabomu ya machozi,kupigwa risasi,kuwatuma mbwa wawang’ate matokeo yake walijeruhiwa vibaya sana..tukio hilo watoto wengi waliuawa.Mungu awalaze pema amin.

Mwaka wa 1991,viongozi wa nchi huru za Afrika chini ya umoja wa nchi huru za Afrika O.A.U. wakapitisha agizo la kuadhimisha siku hii ya juni 16 kuwa ni siku ya kukumbuka maafa ya watoto yaliyotokea Afrika ya kusini.

 Maadhimisho haya yanafanywa Afrika nzima na kuwapa watoto fursa ya kukemea maovu maonevu wanayofanyiwa watoto,watoto kutumia siku hii kudai na kuzungumzia haki zao kwa jamii na serikali kwa ujumla.

 

Kauli mbiu-Kuondoa Mila zenye kuleta madhara ni jukumu letu sote.

 Kumbuka Mila potofu huleta madhara mengi kwa watoto katika njia tofauti.

1.    Tohara kwa watoto wa kike

2.    Ndoa za utotoni

3.    Watoto kushirikishwa katika ngoma za usiku

4.    Jando na unyago usiozingatia maadili n.k

 
Mtoto ni nani?

Mtoto ni yule aliye chini ya umri wa miaka 18. Ila katika ya hapo kuna watoto wadogo zaidi.

Watoto siku zote hawana ugomvi wa kuendelea. Kawaida watoto hawana chuki. Hugombana na mara tena hutafutana na kuendelea kama zamani.

Mtoto anapokuwa katika nyumba huleta faraja kwa kila mmoja aliye ndani. Hata kama utakuwa umekasirika, anapokuja mtoto utajikuta hasira inaondoka na kuanza kucheza naye.

Ili kuamini mtoto mtamu, kuna wanawake wengi ambao Mwenyezi mungu bado hajawajaalia kupata Mtoto. Wamekuwa wakihangaika huku na kule kutafuta mtoto.

Thamani ya mtoto hailinganishwi na jambo lolote.Ndiyo maana wazazi kwa kukosa busara hugombana na hata kufikishana pabaya kisa mtoto wake kapigwa au kanyanyaswa kwa aina yeyote ile.

Hii ni kutokana na thamani kubwa aliyonayo mtoto.Waigizaji maarufu na wenye pesa. Wengi wao walijiingiza katika filamu za watoto baada ya kuona zinavutia zaidi na watu wengi huzipenda.

Vipindi vingi vya watoto vimekuwa vikiwavutiwa watu vikiwa katika Runinga, Radio na hata katika majarida mbalimbali.

Yote haya ni thamani ya mtoto. Tukiangalia kwa waandishi wa Vitabu wengi walielekeza kalamu zao kuandika hadithi za watoto kama ilivyo kwangu. Zimekuwa na soko kwa wakubwa na wadogo.Hii ni thamani ya mtoto.

Ili kujua mtoto ana thamani yakupasa umpe thamani  kwa kuangalia haki mbalimbali za watoto na utende hivyo, utakuwa umemthamini.

 Watoto wana haki ya kusikilizwa

Watoto wanahaki ya kupata Elimu

Watoto wanahaki ya Kupata huduma ya Afya

Watoto wanahaki ya kujaliwa na kupata upendo

Watoto wanahaki ya kutopigwa

Watoto wanahaki ya kupata huduma kwa mahitaji maalum

Watoto wanahaki ya kuishi katika nyumba nzuri

Watoto wana haki ya kupata lishe bora

Watoto wanahaki ya kucheza

Watoto wanahaki ya kushirikishwa katika kufanya maamuzi

Watoto wanahaki ya kuishi bila woga

Watoto wanahaki ya kutolazimishwa kufanya kazi nzito

Watoto wanahaki ya kuheshimiwa kimawazo

Watoto wana haki ya kufundishwa kwa uvumilivu na utulivu

Watoto wanahaki ya kufanya makosa

N.k……

Tutumie siku hii ya mtoto wa Afrika kama changamoto kwetu ya kutafakari na kuchukua hatua nzuri na thabiti katika kulinda hadhi ya mtoto.

Tuwapende na kuwajali. Ndiyo taifa letu la kesho. Mwana umleavyo ndivyo akuavyo.

Jukumu la kusaidia Watoto Yatima

Pongezi kwa  wale wote walio maarufu na wasio maarufu, Masikini kwa matajiri mnaojitolea mlicho nacho kwa ajili ya kusaidia watoto Yatima. Nasema hivyo kwa sababu kutoa ni moyo!. Mtu anaweza akawa nacho kingi lakini asipewe nafasi ya kumfikiria Yatima. Na mtu anaweza pia akawa nacho kidogo naye pia akawa hajajitoa kwa ajili ya Yatima. Kutoa ni moyo.

Asiyenacho kabisa naye pia hajatengwa katika suala la kuhudumia watoto yatima, aidha hata kwa kwenda kituoni au eneo wanaloishi na kuwasalimia huku ukiwapa maneno matamu ya faraja.

Unaweza ukawa nacho kidogo na ukatoa, ukiamini unayempelekea ni mujhitaji zaidi yako, hana hata hicho kidogo. Ndiyo maana kutoa ni moyo.

Mwenyezi Mungu amempa yatima daraja. Hiyo wanadamu ukitoa utegemee malipoyaliyo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Yatima ni mtoto aliyekosa wazazi wawili au mmoja, lakini huyu ni yatima, amepungukiwa na viungo vyake muhimu katika maisha yake.

Tunaamini mzazi ndiyo mlezi wa mtoto, haijalishi masikini au tajiri. Inapotokea akaondoka duniani kwa mapenzi ya Mungu, basi lazima mtoto atayumba. Hakuna jinsi. Iwe anao wa kumsaidia au hana.

Yatima ana hitaji huruma, Upendo na kumpa faraja, ili aweze angalau kujiona jamii iliyo tofauti na wazazi wake nayo inamkubali.

Tuamini kwamba hakuna mwenye funguo ya kuishi milele, wala hakuna anayejua kesho. Ukiwa Mzazi muhurumie Yatima, unaweza ukaondoka na kumuacha mtoto wako au watoto, wakiwa nao yatima. Kama hujazaa basi angalia watu wako wa karibu walioacha watoto yatima kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Kama ni mtoto hana budi kumuhurumia mtoto mwenzake pasipokum’beza, kumnyanyapaa kwa namna yeyote ile, tukiamini watoto wote ni sawa.

Kwa bahati nzuri watoto wa nahaki zao, zinazotambulika kimataifa. Hivyo yatima ni miongoni mwa haki hizo. Kumbuka yatima ni mtoto aliye chini ya umri wa miala 18.

Tukiwa kama wazazi au walezi hatuna budi kupunguza tulicho nacho kwa ajili ya kuwasaidia watoto ambao walezi wake waliobakia ni sisi. Kuna yatima wanaoishi katika vituo ambao msaada wako unauelekeza moja kwa moja kituoni.

Lakini pia kuna wale ambao wanaishi na walezi, lakini ni wahitaji kutokana na hali ya kipato kidogo cha mlezi wake. Msaidie. Kama huna basi muosheshe unamjali kwa maneno matamu.

Kumbuka mmoja ya vitu vinavyoweza kuwaingiza watoto katika kundi la yatima ni kutokana na Mila zenye madhara, ni pamoja na wazazi kurithi mke au mume wa ndugu yake ambaye huenda alifariki kwa maradhi ya maambukizi kama HIV.


 
 
 
 
 

 







rahmamahmoudmk@yahoo.com