Anafahamika kama "JEMBE " ukipenda wanamwita "Tingatinga"
Utendaji na umahiri wake katika kazi na kujiamini. Turufu ya Ccm ktk safari ya Oktoba.
Hongereni kina mama mlio ingia ktk kinyang'anyiro hicho hadi 3 bora. Dr Asharose Migiro aliyonitoa nikafahamika ndani na nje ya nchi kama mwandishi wa Vitabu Mwanamke,baada ya kunizindulia Vitabu vyangu 14,akiwa Waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia na watoto.
TAMWA wakiratibu uzinduzio huo, idara ya habari Maelezo.
Hongera mama Samiya Suluhu Hassan. Ukiwa Ni Mwanamke wa kwanza, kushika nafasi ya Makamu wa rais Tanzania kupitia Ccm.Kila la heri nyote katika kutimiza malengo yenu. Pale Oktoba.
Namkumbuka Mh. Samiya, akiwa Waziri wa Wanawake na Watoto Znz, niliwahi kumualika katika Semina ambayo nilikuwa naratibu
juu Uwandishi wa Vitabu vya fasihi katika kuelimisha gonjwa la UKIMWI. Ilikuwa mahususi kwa Wanawake Waandishi Zanzibar.Asilimia kubwa ya washiriki walikuwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Zanzibar.
Alihudhuria na kutoa mchango mkubwa wa mawazo katika shughuli hiyo.
Hongera Balozi Amina kwa nafasi nzuri hatimaye kushika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro cha urais.Hakika umeonyesha mfano mzuri kwa Wanawake wa Visiwani na bara ktk kujiamini.
Kila la heri mnapoendelea na safari yenu kuelekea Oktoba.
Wanawake wanaweza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni