Aunt Rahma Shopping Centre

Aunt Rahma Shopping Centre
Kariakoo/Tabata Muuzaji wa nguo mbalimbali za watoto na wakubwa kwa bei poa kutoka China na Dubai

Jumanne, 16 Juni 2015

Siku ya Mtoto wa Afrika 2015

 
 

Siku ya Mtoto wa Afrika

 

 

“Kuondoa Mila zenye kuleta madhara ni jukumu letu sote”.

 

Tarehe 16 juni mwaka 1976 Nchini Afrika ya kusini katika kitongozi cha soweto,kulitokea mauaji ya kikatili dhidi ya watoto nchini humo,watoto hao waliouwa wakiwa katika maandamano yaliyokuwa na lengo la kupinga agizo la serikali ya makaburu wakati huo,lillilotaka wanafunzi wafundishwe masomo katika lugha ya kiafrikana badala ya kingereza.

 Watoto  walipinga kufundishwa katika lugha ya kiafrika kwa sababu lugha kiafrikana haizungumzwi na kueleweka mahali popote duniani,zaidi ya Afrika ya kusini tu.

Watoto hao waliona pia lugha hiyo ingeweza kuwakosesha ajira katika nchi nyingine duniani.

 maandamano yao yalitawanywa na polisi wa makaburu kwa kuwatupia mabomu ya machozi,kupigwa risasi,kuwatuma mbwa wawang’ate matokeo yake walijeruhiwa vibaya sana..tukio hilo watoto wengi waliuawa.Mungu awalaze pema amin.

Mwaka wa 1991,viongozi wa nchi huru za Afrika chini ya umoja wa nchi huru za Afrika O.A.U. wakapitisha agizo la kuadhimisha siku hii ya juni 16 kuwa ni siku ya kukumbuka maafa ya watoto yaliyotokea Afrika ya kusini.

 Maadhimisho haya yanafanywa Afrika nzima na kuwapa watoto fursa ya kukemea maovu maonevu wanayofanyiwa watoto,watoto kutumia siku hii kudai na kuzungumzia haki zao kwa jamii na serikali kwa ujumla.

 

Kauli mbiu-Kuondoa Mila zenye kuleta madhara ni jukumu letu sote.

 Kumbuka Mila potofu huleta madhara mengi kwa watoto katika njia tofauti.

1.    Tohara kwa watoto wa kike

2.    Ndoa za utotoni

3.    Watoto kushirikishwa katika ngoma za usiku

4.    Jando na unyago usiozingatia maadili n.k

 
Mtoto ni nani?

Mtoto ni yule aliye chini ya umri wa miaka 18. Ila katika ya hapo kuna watoto wadogo zaidi.

Watoto siku zote hawana ugomvi wa kuendelea. Kawaida watoto hawana chuki. Hugombana na mara tena hutafutana na kuendelea kama zamani.

Mtoto anapokuwa katika nyumba huleta faraja kwa kila mmoja aliye ndani. Hata kama utakuwa umekasirika, anapokuja mtoto utajikuta hasira inaondoka na kuanza kucheza naye.

Ili kuamini mtoto mtamu, kuna wanawake wengi ambao Mwenyezi mungu bado hajawajaalia kupata Mtoto. Wamekuwa wakihangaika huku na kule kutafuta mtoto.

Thamani ya mtoto hailinganishwi na jambo lolote.Ndiyo maana wazazi kwa kukosa busara hugombana na hata kufikishana pabaya kisa mtoto wake kapigwa au kanyanyaswa kwa aina yeyote ile.

Hii ni kutokana na thamani kubwa aliyonayo mtoto.Waigizaji maarufu na wenye pesa. Wengi wao walijiingiza katika filamu za watoto baada ya kuona zinavutia zaidi na watu wengi huzipenda.

Vipindi vingi vya watoto vimekuwa vikiwavutiwa watu vikiwa katika Runinga, Radio na hata katika majarida mbalimbali.

Yote haya ni thamani ya mtoto. Tukiangalia kwa waandishi wa Vitabu wengi walielekeza kalamu zao kuandika hadithi za watoto kama ilivyo kwangu. Zimekuwa na soko kwa wakubwa na wadogo.Hii ni thamani ya mtoto.

Ili kujua mtoto ana thamani yakupasa umpe thamani  kwa kuangalia haki mbalimbali za watoto na utende hivyo, utakuwa umemthamini.

 Watoto wana haki ya kusikilizwa

Watoto wanahaki ya kupata Elimu

Watoto wanahaki ya Kupata huduma ya Afya

Watoto wanahaki ya kujaliwa na kupata upendo

Watoto wanahaki ya kutopigwa

Watoto wanahaki ya kupata huduma kwa mahitaji maalum

Watoto wanahaki ya kuishi katika nyumba nzuri

Watoto wana haki ya kupata lishe bora

Watoto wanahaki ya kucheza

Watoto wanahaki ya kushirikishwa katika kufanya maamuzi

Watoto wanahaki ya kuishi bila woga

Watoto wanahaki ya kutolazimishwa kufanya kazi nzito

Watoto wanahaki ya kuheshimiwa kimawazo

Watoto wana haki ya kufundishwa kwa uvumilivu na utulivu

Watoto wanahaki ya kufanya makosa

N.k……

Tutumie siku hii ya mtoto wa Afrika kama changamoto kwetu ya kutafakari na kuchukua hatua nzuri na thabiti katika kulinda hadhi ya mtoto.

Tuwapende na kuwajali. Ndiyo taifa letu la kesho. Mwana umleavyo ndivyo akuavyo.

Jukumu la kusaidia Watoto Yatima

Pongezi kwa  wale wote walio maarufu na wasio maarufu, Masikini kwa matajiri mnaojitolea mlicho nacho kwa ajili ya kusaidia watoto Yatima. Nasema hivyo kwa sababu kutoa ni moyo!. Mtu anaweza akawa nacho kingi lakini asipewe nafasi ya kumfikiria Yatima. Na mtu anaweza pia akawa nacho kidogo naye pia akawa hajajitoa kwa ajili ya Yatima. Kutoa ni moyo.

Asiyenacho kabisa naye pia hajatengwa katika suala la kuhudumia watoto yatima, aidha hata kwa kwenda kituoni au eneo wanaloishi na kuwasalimia huku ukiwapa maneno matamu ya faraja.

Unaweza ukawa nacho kidogo na ukatoa, ukiamini unayempelekea ni mujhitaji zaidi yako, hana hata hicho kidogo. Ndiyo maana kutoa ni moyo.

Mwenyezi Mungu amempa yatima daraja. Hiyo wanadamu ukitoa utegemee malipoyaliyo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Yatima ni mtoto aliyekosa wazazi wawili au mmoja, lakini huyu ni yatima, amepungukiwa na viungo vyake muhimu katika maisha yake.

Tunaamini mzazi ndiyo mlezi wa mtoto, haijalishi masikini au tajiri. Inapotokea akaondoka duniani kwa mapenzi ya Mungu, basi lazima mtoto atayumba. Hakuna jinsi. Iwe anao wa kumsaidia au hana.

Yatima ana hitaji huruma, Upendo na kumpa faraja, ili aweze angalau kujiona jamii iliyo tofauti na wazazi wake nayo inamkubali.

Tuamini kwamba hakuna mwenye funguo ya kuishi milele, wala hakuna anayejua kesho. Ukiwa Mzazi muhurumie Yatima, unaweza ukaondoka na kumuacha mtoto wako au watoto, wakiwa nao yatima. Kama hujazaa basi angalia watu wako wa karibu walioacha watoto yatima kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Kama ni mtoto hana budi kumuhurumia mtoto mwenzake pasipokum’beza, kumnyanyapaa kwa namna yeyote ile, tukiamini watoto wote ni sawa.

Kwa bahati nzuri watoto wa nahaki zao, zinazotambulika kimataifa. Hivyo yatima ni miongoni mwa haki hizo. Kumbuka yatima ni mtoto aliye chini ya umri wa miala 18.

Tukiwa kama wazazi au walezi hatuna budi kupunguza tulicho nacho kwa ajili ya kuwasaidia watoto ambao walezi wake waliobakia ni sisi. Kuna yatima wanaoishi katika vituo ambao msaada wako unauelekeza moja kwa moja kituoni.

Lakini pia kuna wale ambao wanaishi na walezi, lakini ni wahitaji kutokana na hali ya kipato kidogo cha mlezi wake. Msaidie. Kama huna basi muosheshe unamjali kwa maneno matamu.

Kumbuka mmoja ya vitu vinavyoweza kuwaingiza watoto katika kundi la yatima ni kutokana na Mila zenye madhara, ni pamoja na wazazi kurithi mke au mume wa ndugu yake ambaye huenda alifariki kwa maradhi ya maambukizi kama HIV.


 
 
 
 
 

 







rahmamahmoudmk@yahoo.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni