Siku ya Mtoto wa Afrika
“Kuondoa Mila zenye kuleta madhara ni jukumu letu
sote”.
Tarehe 16 juni mwaka 1976
Nchini Afrika ya kusini katika kitongozi cha soweto,kulitokea mauaji ya
kikatili dhidi ya watoto nchini humo,watoto hao waliouwa wakiwa katika maandamano
yaliyokuwa na lengo la kupinga agizo la serikali ya makaburu wakati
huo,lillilotaka wanafunzi wafundishwe masomo katika lugha ya kiafrikana badala
ya kingereza.
Watoto hao waliona pia lugha
hiyo ingeweza kuwakosesha ajira katika nchi nyingine duniani.
Mwaka wa 1991,viongozi wa nchi
huru za Afrika chini ya umoja wa nchi huru za Afrika O.A.U. wakapitisha agizo
la kuadhimisha siku hii ya juni 16 kuwa ni siku ya kukumbuka maafa ya watoto
yaliyotokea Afrika ya kusini.
Kauli mbiu-Kuondoa Mila zenye
kuleta madhara ni jukumu letu sote.
Kumbuka Mila
potofu huleta madhara mengi kwa watoto katika njia tofauti.
1. Tohara
kwa watoto wa kike
2.
Ndoa za utotoni
3.
Watoto kushirikishwa katika ngoma za usiku
4. Jando
na unyago usiozingatia maadili n.k
Mtoto ni yule aliye chini ya umri wa miaka 18. Ila katika ya hapo
kuna watoto wadogo zaidi.
Watoto siku zote hawana ugomvi wa kuendelea. Kawaida watoto hawana
chuki. Hugombana na mara tena hutafutana na kuendelea kama zamani.
Mtoto anapokuwa katika nyumba huleta faraja kwa kila mmoja aliye
ndani. Hata kama utakuwa umekasirika, anapokuja mtoto utajikuta hasira
inaondoka na kuanza kucheza naye.
Ili kuamini mtoto mtamu, kuna wanawake wengi ambao Mwenyezi mungu
bado hajawajaalia kupata Mtoto. Wamekuwa wakihangaika huku na kule kutafuta
mtoto.
Thamani ya mtoto hailinganishwi na jambo lolote.Ndiyo maana wazazi
kwa kukosa busara hugombana na hata kufikishana pabaya kisa mtoto wake kapigwa
au kanyanyaswa kwa aina yeyote ile.
Hii ni kutokana na thamani kubwa aliyonayo mtoto.Waigizaji maarufu
na wenye pesa. Wengi wao walijiingiza katika filamu za watoto baada ya kuona
zinavutia zaidi na watu wengi huzipenda.
Vipindi vingi vya watoto vimekuwa vikiwavutiwa watu vikiwa katika
Runinga, Radio na hata katika majarida mbalimbali.
Yote haya ni thamani ya mtoto. Tukiangalia kwa waandishi wa Vitabu
wengi walielekeza kalamu zao kuandika hadithi za watoto kama ilivyo kwangu.
Zimekuwa na soko kwa wakubwa na wadogo.Hii ni thamani ya mtoto.
Ili kujua mtoto ana thamani yakupasa umpe thamani kwa kuangalia haki mbalimbali za watoto na
utende hivyo, utakuwa umemthamini.
Watoto wanahaki ya kupata Elimu
Watoto wanahaki ya Kupata huduma ya Afya
Watoto wanahaki ya kujaliwa na kupata upendo
Watoto wanahaki ya kutopigwa
Watoto wanahaki ya kupata huduma kwa mahitaji maalum
Watoto wanahaki ya kuishi katika nyumba nzuri
Watoto wana haki ya kupata lishe bora
Watoto wanahaki ya kucheza
Watoto wanahaki ya kushirikishwa katika kufanya maamuzi
Watoto wanahaki ya kuishi bila woga
Watoto wanahaki ya kutolazimishwa kufanya kazi nzito
Watoto wanahaki ya kuheshimiwa kimawazo
Watoto wana haki ya kufundishwa kwa uvumilivu na utulivu
Watoto wanahaki ya kufanya makosa
N.k……
Tutumie siku hii ya mtoto wa Afrika kama changamoto kwetu ya
kutafakari na kuchukua hatua nzuri na thabiti katika kulinda hadhi ya mtoto.
Tuwapende na kuwajali. Ndiyo taifa letu la kesho. Mwana umleavyo
ndivyo akuavyo.
Jukumu
la kusaidia Watoto Yatima
Pongezi
kwa wale wote walio maarufu na wasio
maarufu, Masikini kwa matajiri mnaojitolea mlicho nacho kwa ajili ya kusaidia
watoto Yatima. Nasema hivyo kwa sababu kutoa ni moyo!. Mtu anaweza akawa nacho
kingi lakini asipewe nafasi ya kumfikiria Yatima. Na mtu anaweza pia akawa
nacho kidogo naye pia akawa hajajitoa kwa ajili ya Yatima. Kutoa ni moyo.
Asiyenacho
kabisa naye pia hajatengwa katika suala la kuhudumia watoto yatima, aidha hata
kwa kwenda kituoni au eneo wanaloishi na kuwasalimia huku ukiwapa maneno matamu
ya faraja.
Unaweza
ukawa nacho kidogo na ukatoa, ukiamini unayempelekea ni mujhitaji zaidi yako,
hana hata hicho kidogo. Ndiyo maana kutoa ni moyo.
Mwenyezi
Mungu amempa yatima daraja. Hiyo wanadamu ukitoa utegemee malipoyaliyo makubwa
kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Yatima
ni mtoto aliyekosa wazazi wawili au mmoja, lakini huyu ni yatima, amepungukiwa
na viungo vyake muhimu katika maisha yake.
Tunaamini
mzazi ndiyo mlezi wa mtoto, haijalishi masikini au tajiri. Inapotokea akaondoka
duniani kwa mapenzi ya Mungu, basi lazima mtoto atayumba. Hakuna jinsi. Iwe
anao wa kumsaidia au hana.
Yatima
ana hitaji huruma, Upendo na kumpa faraja, ili aweze angalau kujiona jamii
iliyo tofauti na wazazi wake nayo inamkubali.
Tuamini
kwamba hakuna mwenye funguo ya kuishi milele, wala hakuna anayejua kesho. Ukiwa
Mzazi muhurumie Yatima, unaweza ukaondoka na kumuacha mtoto wako au watoto,
wakiwa nao yatima. Kama hujazaa basi angalia watu wako wa karibu walioacha
watoto yatima kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Kama
ni mtoto hana budi kumuhurumia mtoto mwenzake pasipokum’beza, kumnyanyapaa kwa
namna yeyote ile, tukiamini watoto wote ni sawa.
Kwa
bahati nzuri watoto wa nahaki zao, zinazotambulika kimataifa. Hivyo yatima ni
miongoni mwa haki hizo. Kumbuka yatima ni mtoto aliye chini ya umri wa miala
18.
Tukiwa
kama wazazi au walezi hatuna budi kupunguza tulicho nacho kwa ajili ya
kuwasaidia watoto ambao walezi wake waliobakia ni sisi. Kuna yatima wanaoishi
katika vituo ambao msaada wako unauelekeza moja kwa moja kituoni.
Lakini
pia kuna wale ambao wanaishi na walezi, lakini ni wahitaji kutokana na hali ya
kipato kidogo cha mlezi wake. Msaidie. Kama huna basi muosheshe unamjali kwa
maneno matamu.
Kumbuka
mmoja ya vitu vinavyoweza kuwaingiza watoto katika kundi la yatima ni kutokana
na Mila zenye madhara, ni pamoja na wazazi kurithi mke au mume wa ndugu yake
ambaye huenda alifariki kwa maradhi ya maambukizi kama HIV.
rahmamahmoudmk@yahoo.com