Makala
Historia ya Mwanariadha maarufu asiyeona
Henry Wanyoike aliyezaliwa
mwaka 1974 ni Mwanariadha wa
Kenya asiyeona. Anashiriki katika mashindano ya Paralympics shindano la Marathon.
Wanyoike ni mmoja wa Wanariadha wa kasi sana duniani.
Alianza kukimbia akiwa mtoto na tayari alikuwa na ndoto ya kujiunga na kundi la
Kenya la
wanariadha.
Nchi hiyo inajulikana kwa kuwakuza Wanariadha wengi wa
Masafa marefu wa Kimataifa kuliko nchi nyingine yoyote.
Alitia fora katika mita 5000 na mita 10,000.
Mnamo 1995, Wanyoike alikuwa kipofu wakati alipata
mshtuko. Alisimulia,alieleza kwamba alienda kitandani akiwa mzima, kuamka
aliona giza machoni pake. Usiku huo alipoteza karibu asilimia 95 ya uwezo wake
wa kuona na polepole akiupoteza wote. Alifikiria akaona maisha yake yamefika
kikomo.
Mamaye Grace alimchukua katika kliniki ya macho ya Kikuyu inayotambulika kama moja ya vituo bora zaidi vya watu
walio na shida ya macho katika eneo la Afrika Mashariki.
Msimamizi wa mradi wa Low Vision alimsaidia
kujipanga tena kimaisha na akampanga kujifunza kushona fulana. Kwa shukrani
kubwa alikubali mradi huo na kuahidi kuwasaidia vipofu wengine kujitegemea
kimaisha .
Baada ya kushinda Nishani ya Dhahabu kule Sydney, Australia
katika Mashindano ya Paralympic ya 2000, Wanyoike
amenunua mashine nyingi za kushona kutokana na zawadi ya fedha alizokabidhiwa
na watu maarufu kama vile Arnold Schwarzenegger. Akawa ni mwajiri
wa watu wengine vipofu wa Kenya na kuwafundisha kufuma fulana.
Mwanariadha kopofu huwa na mtu wa kumwongoza
aliyefunganishwa naye mkononi. Kiongozi hutumia kiunganishi hiki kumwashiria
mwanariadha, bila kumzidi kasi, wakati wa kugeuka, kupunguza kasi na kuhepa
kizuizi, iwe kiwanjani au barabarani.
Henry alipozoea kushirikiana na viongoza, alichipuka
haraka kama mwanariadha kipofu wa kimataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni