Aunt Rahma Shopping Centre

Aunt Rahma Shopping Centre
Kariakoo/Tabata Muuzaji wa nguo mbalimbali za watoto na wakubwa kwa bei poa kutoka China na Dubai

Jumapili, 20 Desemba 2015

Msanii Pawpaw ajenga hoteli ya kifahari





Nimekuwa nikivutiwa sana na uigizaji wa wasanii wa Nigeria Osita Iheme "Pawpaw" na mwenzake, wanapo kuwa ktk filamu. Wanavaa uhusika kuanzia mavazi mpaka wanavyojiweka.Huwezi amini ukiambiwa hawa ni matajiri.


Hii inatoa changamoto kwa waigizaji kuvaa uhusika halisi.Siyo kila filamu Uwe umevaa tofauti na kile kilichokusudiwa.

Nimevutiwa kuona jinsi wanavyopata thamani hadi kufanikiwa Pawpaw kujenga hotel ya kifahari Nchini kwao Nigeria

Hotel hiyo ya ghorofa kadhaa kaijenga kwa miezi saba miji Imo.Aliizindua akishirikiana na wasanii wenzake pamoja na wanamuziki.




Jumanne, 1 Desemba 2015

Mtoto wa miaka 10, ajifungua Mtoto




Wakati wanaharakati mbali mbali duniani wakipambana kupinga ukatili kwa watoto,
huko nchini Kenya mtoto wa miaka 10 ambaye angetakiwa kuwa shuleni akisoma na kucheza na wenzake michezo mbali mbali, anapata jukumu la kumlea mtoto mwenzake.  

Gladys chelagat  alijifungua mtoto wake wa kiume mwenye uzito wa kg 2.8 katika hospital ya kericho nchini kenya.Hata.

.Hata hivyo Mungu ni mkubwa kwani pamoja na udogo wa mtoto huyu alijifungua salama bila ya kupata tatizo lolote la kiafya.

Jumanne, 17 Novemba 2015

Peruzi-Magazeti
















RAIS MTATA WA AFRIKA MH MUGABE AMLIPUA RAILA ODINGA

 
 
 
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemshambulia kwa maneno mwanasiasa mkongwe wa Kenya ambaye pia ni kiongozi wa chama cha CORDS huku akimpiga marufuku kukanyaga ardhi ya nchi hiyo.
Akizungumza huko Marondela katika hafla iliyowahusisha wanajeshi walioshiriki katika vita mbalimbali, Mugabe alimtuhumu Raila kwa kutaka kumpindua kwenye nafasi yake kwa kuwapandikiza wapinzani nchini humo.
Hivi ndivyo alivyosema:
“Raila Odinga is mwanasiasa muongo wa Kenya, mwanaume mnafiki ambaye yuko katika mkiakati wa kuwapandikiza marafiki zake kuwa marais kwenye nchi zote za Afrika ili awe mwenyekiti mwenye nguvu kwenye Umoja wa Afrika (AU), siku moja watamuangusha kwenye sanduku la kura.
“Angalia alichokifanya Nigeria, Tanzania, Ivory Coast na anataka kufanya hivyo pia Uganda kwa kumtumia rafiki yake Kiiza Besigye ambaye leo anapewa sifa na ushupavu ambao anapata kutokana tu na amri za Raila barani Afrika.
“Hapa hatutamruhusu kuwageuza marafiki zake wa zamani Tendai Biti na Morgan kuniondoa mimi, hakuna kwa namna yoyote. Nitatawala kwa miaka 90 zaidi. Nimeikiamuru kikosi maalum cha jeshi kuangusha ndege yoyote itakayokuwa imembeba huyo mwendawazimu Raila na kundi lake la mipango ya uchakachuaji wa kura dhidi ya marais wanaoendelea kutawala Afrika.
“Nimewaamuru walinzi wangu kuhakikisha wanakuwa makini kuhakikisha Raila hajipenyezi bila kubainika.
“Tutashindwaje kukosa usingizi kwa sababu tu ya Raila, yeye ni kitu gani? Tutamkamata na kumhasi kabla yeye na timu yake hawajamsaidia Morgan na Biti kunipindua kwenye Urais.”
Hii sio mara ya kwanza kwa Mugabe kushambulia Kenya kwa maneno, wiki chache zilizopita alidai kuwa wananchi wa Kenya ni wezi kutoka damuni na kwamba anadhani wanasomea shahada ya wizi. Alitahadharisha wananchi wake kutokubali kukaa karibu na wakenya kwa madai kuwa wanaweza kuwaambukiza wizi.
Mwezi Juni mwaka 2008, Raila Odinga aliwasilisha pendekezo lake mbele ya Umoja wa Afrika akitaka Umoja huo kumsimamisha uanachama Rais Mugabe hadi pale atakaporuhusu uchaguzi wa huru na haki nchini kwake.
Chanzo- Wananchi blog.
 

Jumatatu, 16 Novemba 2015

Mtoto mwenye kipaji cha Ajabu


Wakati kina mama wananunua simu, njema anazamia mfukoni-Jionee


Kina mama na Vipaji vya wizi-Jionee


Mwandishi wa Vitabu aliyefukuzwa shule na wakoloni


 Makala

“Mongo Beti Mwandishi aliyefukuzwa shule kwa kukaidi sheria za wakoloni”

Alexandra biyidi Awala  ni muandishi maarufu wa Vitabu nchini kameruni na katika bara la Africa.

Jina lake maarufu la uandishi wa vitabu ni Mongo beti. Alizaliwa juni 30 mwaka 1932 nchini kameruni , katika kijiji kidogo cha Akometan, kilichopo kilometa 10 kutoka mbalmayo, ambapo ni kilometa 45 kutoka mji mkuu wa yuonde.

Mongo beti alikuwa mpinzani mkubwa ukoloni na dini zao. Na hata alifukuzwa katika shule ya misheni.Yeye alichotaka kila jambo litoke kwa waafrika mila na desturi zetu ndiyo ziwe dira.

 Alipitia kitabu maarufu cha black child (Mtoto wa kiafrika) ambacho kilikuwa kinatumika mashuleni katika fasihi za kingereza barani afrika. Kilichotungwa na muandishi maarufu kamara leya.

Vitabu vya Mango Beti viliandikwa katika lugha ya kifaransa, moja ya kitabu chake nikikitafsiri katika lugha yetu ya Kiswahili kinaitwa mkono wa kikatili, dhidi ya wakameruni.

Maandiko yake yalilenga katika kumkomboa muafrika kifikra na ustawi wa bara la Afrika na muafrika mwenyewe.

Huyo ndiye Alexandra biyidi Awala alimaarufu Mongo Beti, kutoka nchini Kameruni.

Jamhuri ya Kamerun :

 Ni Jamhuri ya umoja katika Afrika ya Magharibi. Imepakana na Nigeria, Chadi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Guinea ya Ikweta na Guba ya Guinea.

Kamerun ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kukabidhiwa.

Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kamerun ikawa nchi huru, na kuungana na eneo la Kamerun ya Uingereza mwaka 1961 kuunga kwa Shirikisho la Jamhuri ya Kamerun. Na baadaye kubadilisha jina kwa Jamhuri ya Muungano ya Kamerun mwaka wa 1972, na baadaye ikawa Jamhuri ya Kamerun ama kwa KifaransaRépublique du Cameroun mwaka  1984. Lugha rasmi na lugha za taifa ni Kiingereza na Kifaransa

 

 

Vichekesho vya mtandao


Vichekesho vya mtandao

Kulikua na wapenzi wawili walikua wanapendana Sana Siku Moja wakaamua wafe Pamoja. Wakapanda Gorofan Hadi Juu wakakimbia kwakasi mwanaume akajirusha mwanamke akasita akasema afadhali ufe kwamaana Sikupendi, kabla Yule Mwaume Ajafika chini akatoa parachuti alafu akasema unabahati sana ungekufa wewe!

Swali : Jee Kuna Upendo wa Kweli hapo?

 

Jumamosi, 17 Oktoba 2015

Matukio ya msiba wa Mbunge Filikunjombe na wenzake

                               Mke wa Marehemu Filikunjombe akiwa na wanawe