Makala
“Mongo Beti
Mwandishi aliyefukuzwa shule kwa kukaidi sheria za wakoloni”
Alexandra biyidi Awala ni
muandishi maarufu wa Vitabu nchini kameruni na katika bara la Africa.
Jina lake maarufu la uandishi wa vitabu ni Mongo beti. Alizaliwa
juni 30 mwaka 1932 nchini kameruni , katika kijiji kidogo cha Akometan,
kilichopo kilometa 10 kutoka mbalmayo, ambapo ni kilometa 45 kutoka mji mkuu wa
yuonde.
Mongo beti alikuwa mpinzani mkubwa ukoloni na dini zao. Na hata
alifukuzwa katika shule ya misheni.Yeye alichotaka kila jambo litoke kwa
waafrika mila na desturi zetu ndiyo ziwe dira.
Alipitia kitabu maarufu cha
black child (Mtoto wa kiafrika) ambacho kilikuwa kinatumika mashuleni katika
fasihi za kingereza barani afrika. Kilichotungwa na muandishi maarufu kamara
leya.
Vitabu vya Mango Beti viliandikwa katika lugha ya kifaransa, moja
ya kitabu chake nikikitafsiri katika lugha yetu ya Kiswahili kinaitwa mkono wa
kikatili, dhidi ya wakameruni.
Maandiko yake yalilenga katika kumkomboa muafrika kifikra na ustawi
wa bara la Afrika na muafrika mwenyewe.
Huyo ndiye Alexandra biyidi Awala alimaarufu Mongo Beti, kutoka
nchini Kameruni.
Jamhuri ya Kamerun :
Ni Jamhuri ya
umoja katika Afrika ya
Magharibi. Imepakana na Nigeria, Chadi, Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Guinea
ya Ikweta na Guba ya Guinea.
Kamerun ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita
Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani
kushindwa vita nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini
ya mamlaka ya Shirikisho
la Mataifa kama eneo la kukabidhiwa.
Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kamerun ikawa nchi huru, na kuungana na
eneo la Kamerun ya Uingereza mwaka 1961 kuunga kwa Shirikisho la Jamhuri ya Kamerun. Na
baadaye kubadilisha jina kwa Jamhuri ya Muungano ya Kamerun mwaka wa 1972, na baadaye ikawa Jamhuri ya Kamerun ama kwa KifaransaRépublique du Cameroun mwaka 1984. Lugha rasmi na lugha za taifa ni Kiingereza na Kifaransa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni